Sunday, September 21, 2014

ELIMU YA MAANDALIZI

HAPA NDIPO TUNAPOPAKOSEA hadi kufikia mtoto kushindwa kusoma na kuandika hadi kufika sekondari.

Thursday, August 22, 2013

ELIMU YA TANZANIA
"Elimu ni ufunguo wa maisha" huu ni msemo unaotumiwa kama SLOGAN kwa elimu ya Tanzania, ni msemo uliotoholea kutoka lugha ya kingereza "education is the key to life"
Suala la msingi la kujiuliza Jee hii elimu tunayopewa watanzania  ndio ufunguo wa Maisha?
Jibu lipo katika akili ya kila mmoja wetu, inawezekana jibu likawa "ndio", "hapana" au "sijui"

HALI HALISI
Mwanafunzi anaanza shule za maandalizi  kwa miaka miwili
Anaendelea na Shule ya Msingi kwa muda wa miaka saba
Anaendelea na Shule ya Secondari kwa miaka minne (O'LEVEL)
Anaendelea na Shule ya Secondari ya juu miaka miwili (A'LEVEL)
Anaendelea na elimu ya juu (Certificate, Diploma, na Degree)

jee mara babda ya kumaliza viwango hivyo vya elimu mwanafunzi anaweza kuitumia elimu yake kutumikia jamii iliyomsomesha na inayomtarajia?
majibu pia yapo vichwani mwa msomaji wa ujumbe huu.

mwanafunzi anamaliza na kufaulu darasa la saba na kuingia kidato cha kwanza lakini hajui kusoma na kuandika kiswahili achilia mbali kingereza ambayo ni lugha ya kigeni.

mwanafunzi anamaliza ENGINEERING DEGREE lakini hawezi hata kutengeneza toys la gari seuze gari lenyewe

mwanafunzi anamaliza degree ya Sayansi lakini hawezi kufundisha  somo la physics, chemistry, biology au Mathematics hata ngazi ya kidato cha pili, hapa kunaashiria nini?

TAFAKARI..... CHUKUA.... HATUA